Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS)

Mfumo wa ILMIS utaongeza usalama wa ardhi na pia kutakuwa na mabadiliko makubwa kwa wafanyakazi, wateja na wadau wengine wote. Kukosekana kwa taarifa muhimu na sahihi inasababisha kuwepo kwa mkanganyiko na Imani potofu, kukosa uaminifu na inachangia kuwepo kwa utomvu wa nidhamu na maadili nakusababisha udanganyifu; kwa kifupi, watu hawana Imani na mfumo uliopo wa usimamizi wa ardhi.

Mradi huu mpya,thabiti na wakuaminika wa ILMIS utaimarisha yafuatayo:

1. Utaongeza usalama wa umiliki wa ardhi,

2. kutoa huduma rahisi, yakuaminika na salama kwa mteja

3. Kupunguza muda wakukagua, kusahihisha na kubadilisha ama kuhamisha umiliki wa ardhi,

4. Kupunguza uvamizi wa ardhi, misitu, hifadhi za barabara na sehemu za wazi,

5. uhifadhi wa ardhi na maliasili

6. Kupunguza rushwa na viashiria vyote vya rushwa hususani wakati wa ufuatiliaji, usajili na uhamisho wa hati miliki,

© 2016 Haki zote zimehifadhiwa | Onyo | RAMANI YA TOVUTI