Madhumuni makubwa ya kuanzishwa kwa mradi huu wa ILMIS ni kuongeza na kuimarisha usalama wa umiliki wa ardhi kwa kuboresha shughuli zote zinazohusiana na ardhi kwa ufanisi mkubwa. Pia wateja kupatiwa huduma stahiki kwa haraka, na kuwarudishia Imani wananchi na kuwahakikishia kuwa maswala yote yanayohusiana na ardhi kote nchini, yanashughulikiwa kwa umakini mkubwa sasa hivi kuliko ilivyokuwa awali.
Mfumo unganishi wa taarifa za ardhi (ILMIS) utafanikisha yafuatayo:
1. Kuimarisha utunzaji wa kumbukumbu na kuongeza usalama wa umiliki wa ardhi .
2. Kusimamia usambazaji wa taarifa za ardhi zilizo sahihi na nafuu kwa kuboresha viwango vya huduma kwa wateja kote nchini na kwa haraka zaidi..
3. Kupunguza muda wa usajili, ukaguzi, uhakiki, ama ubadilishaji wa umiliki wa ardhi endapo itahitajika.
4. Kuzuia na kudhibiti uvamizi wa maeneo ya hifadhi ya maji, misitu, maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya barabara pamoja na maeneo mengine ya umma.
5. Kuboresha usimamizi wa ardhi na maliasili.
6. Mradi pia utakupunguza ama kuondoa kabisa urasimu na mianya na viashiria vyote vya rushwa hususani wakati wa kuhakiki, kusajili na kuhamisha hati miliki ya ardhi.
7. Kuwajengea wananchi Imani kuwa mfumo mpya wa usimamizi na utawala wa ardhi ni makini na wa kuaminika.
IMradi wa ILMIS ulianza Mwezi Julai 2016 na utakamilika Mwezi Julai 2018 ikiwa ni pamoja na kipindi cha maandalizi ya mradi .
Utekelezaji wa awali wa mradi wa ILMIS utaanzia Mkoa wa Dar es Salaam katika Ofisi za Kanda ya Dar es Salaam na katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
1 Mtaa wa Ardhi
Kivukoni
S.L.P 9132
11477 Dar Es Salaam, Tanzania
ps@ardhi.go.tz
www.ardhi.go.tz
© 2016 Haki zote zimehifadhiwa | Onyo | RAMANI YA TOVUTI