IGN FI

Imeanzishwa mwaka 1986 na Makao Makuu yake ni Paris, IGN FI inatambulika dunia nzima kwa ufanisi wake katika masuala ya taarifa za kijografia na mitazamo yake chanya katika matumizi na ulindaji wa taarifa za kijografia. Kampuni ya IGN FI inatoa zana saidizi katika kufanya maamuzi kwa lengo la kusimamia mambo ya ardhi, usajili, mipango miji, mazingira, kilimo, usalama wa kiraia, kumudu changamoto/hatari, usafiri, na utalii.

IGN FI ni sehemu ya muunganiko wa makampuni ya GEOFIT na ni mutekelezaji wa IGN France katika kuendesha miradi ya kimataifa. Kampuni inatoa msaada wa kitaalam katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za: upimaji, metrolojia, utengenezaji ramani, mfumo wa taarifa (database), mifumo ya taarifa za kijografia, maonesho ya kimazingira, na mifumo ya taarifa za ardhi.

Kampuni inauzoefu mkubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayohusu na usimamizi wa makusanyo ya fedha zinazotokana na ada na tozo za huduma mbalimbali za ardhi, kuweka mifumo ya kisasa ya ramani za taifa, usimamizi wa ardhi na usajili, ufafanuzi wa mipaka, utekelezaji wa mipango ya taifa ya kijometiki, utunzajia mazingira, kuunda mfumo wa taarifa za kimazingira, usimamizi wa metrologikia katika sehemu hatarishi, uanzishaji wa vituo vya kupambana na majanga ya kimazingira, kilimo/misitu, usalama wa kiraia/ulinzi na nishati. IGN FI inafanyakazi kimataifa ikiwa na waakilishi na washirika karibu duniani kote ikiwemo.:

  • Asia: Indonesia, Mongolia, Vietnam, Cambodia, Myanmar, Ufilipino

  • Mashariki ya Kati: Saudi Arabia, Oman, Falme za Kiarabu, Kuwait, Bahrain

  • Maghreb: Algeria, Morocco, Libya, Lebanon

  • Afrika Magharibi: Mauritania, Senegal, Burkina Faso, Niger

  • Afrika ya kati: Chad, DRC, Congo, Gabon, Cameroon

  • Mashariki na Kusini Mwaafrika: Ethiopia, Uganda, Sudan, Tanzania, Zimbabwe, Zambia, Botswana

  • Amerika Kusini: Brazil

© 2016 Haki zote zimehifadhiwa | Onyo | RAMANI YA TOVUTI