Mradi wa ILMIS umetangazwa sana kwenye vyombo vya habari vya runinga na magazeti. Magazeti ya ndani ya lugha ya Kiswahili Mwananchi, Nipashe na Habari Leo kwa kiasi kikubwa wameripoti habari za mradi wa ILMIS, na magazeti ya lugha ya kiingereza The Citizen, The Guardian, Star TV na The Daily News.
Vituo vinne vya runinga ikiwa ni pamoja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), ITV, na Channel Ten kwa kiasi kikubwa wametangaza ujio wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi (MLHHSD) katika Kituo cha Taifa cha Ardhi (NLIC) 27/11/2017 pamoja na kutangaza mambo mbalimbali yahusiyo mradi wa ILMIS ikiwemo na warsha za uwezeshaji ilofanyika 24/11/2017. TBC kwa sasa inaadaa makala kuhusu mradi wa ILMIS itakayorushwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuanzia februari 2018.
© 2016 Haki zote zimehifadhiwa | Onyo | RAMANI YA TOVUTI