Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS)

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishirikiana na Makampuni ya IGN FI/IGN/ FIT Conseil na Memories (Taasisi ya Kitaifa ya Nchini Ufaransa inayoshughulika na ukusanyaji wa taarifa za Kigeographia na Misitu); kwa pamoja unatekeleza mradi wa kubuni, kusambaza, kusimika na kutekeleza mfumo unganishi wa taarifa za ardhi - Integrated Land Management Information System kwa lugha ya ufupisho utajulikana kama (ILMIS) uloanza Julai 2016 na utaisha Julai 2018.

Utekelezaji wa mradi huu ni moja moja ya sehemu kubwa ya utekelezaji wa miradi ya ushindani ya sekta binafsi (AF – PSCP) ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania, ukiwa ni kama mradi wa jumla wa maendeleo unaolenga kuimarisha mazingira ya kibiashara nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na mabadiliko katika umiliki wa ardhi na kuongeza mianya katika kupata huduma za kifedha. AF – PSCP inalenga kutatua changamoto zinazoikumba sekta ya ardhi kwa kutoa huduma bora za ardhi kwa umma. Mradi wa ILMIS unatarajiwa kushughulikia masuala yote ya sekta ya ardhi, kutoa muongozo katika kuyashughulikia matatizo yote ya ardhi. Kuboresha usalama na uhakika katika manunuzi ya ardhi kupitia taarifa salama na za uhakika, kutoa muongozo wa kiufundi katika kutoa taarifa za ardhi, kusimamia ufanisi wa utoaji wa huduma za ardhi kwa umma. Mradi wa ILMIS utachangia katika uhakika wa usimamizi wa ardhi na huduma za uhakika kwa wateja na kuongeza imani ya wananchi katika utoaji wa huduma za ardhi.

© 2016 Haki zote zimehifadhiwa | Onyo | RAMANI YA TOVUTI