Semina ya ILMIS

Semina iloitwa “Utangulizi kuhusu mradi wa Mfumo Unganishi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS)” ilifanyika hotel ya Kilimanjaro Hyatt, Dar es Salaam tarehe 24/11/2017. Lengo kuu la semina hiyo ni kuuelezea mradi wa ILMIS kwa wawakilishi wa jiji la dar es salaam, pamoja na manispaa ya Ubungo na Kinondoni. Semina iliendeshwa na mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni ili kukuza uwelewa na faida za mradi wa ILMIS miongoni mwa wadau muhimu wa mradi walioshiriki akiwemo naibu katibu mkuu wa wizara ya fedha Dorothy Mwaniyika.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (MLHHSD) imeingia makubaliano na kampuni ya IGN FI kwenye ubunifu wa hatua za majaribio, usambazaji, uanzishaji, na usimikaji wa Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS) kwa msaada wa Benki ya Dunia. Mradi umeanza kutekelezwa katika ofisi za Wizara ya Ardhi, kanda ya Dar es Salaam, na katika hatua za majaribio umeanza katika Manispaa za ubungo na Kinondoni, ILMIS itahusika kikamilifu kuunganisha Idara ya Msajili (RTU), Idara ya Ardhi, na Idara ya Upimaji na Ramani (SMD). Pia itasaidia kwenye mchakato wa ubadilishaji wa taarifa za ardhi na ramani kuziweka kidijitali. Utekelezaji wa mradi ulianza mwezi Agosti, 2016 na ni mradi wa miaka miwili mpaka mwezi Agosti, 2018, ikifuatiwa na mwaka mmoja wa usimamizi kabla ya kutekelezwa nchi nzima katika awamu ya pili ya mradi.

Semina ya kwanza ya kujenga uwezo ilifanyika tarehe 29/09/2017 katika hoteli ya New Africa Dar es Salaam na ililenga kukuza uwelewa juu ya dhana ya ILMIS na mambo muhimu na takribani viongozi wa juu 50 kutoka wizara ya ardhi (MLHHSD) walishiriki na wadau wa nje kutoka wizara mbalimbali, wakala wa serikali na taasisi za umma.

© 2016 Haki zote zimehifadhiwa | Onyo | RAMANI YA TOVUTI