Masuala ya Ardhi Tanzania

Swala la usimamizi wa ardhi Tanzania ni moja ya masuala yaliopewa kipaombele na ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi. Upatikanaji, Umiliki na Usalama wa Ardhi nchini ni mojawapo ya maeneo yaliyopewa kipaumbele katika utekelezaji wa majukumu Kitaifa na pia ni eneo lililowekewa msisitizo mkubwa katika Mpango wa Kitaifa wa Maendeleo ndani ya Miaka Mitano yaani Five Years Development Plan (FYDP) 2016/17 – 2020/21. Kupunguzwa au kuondolewa kwa migogoro inayohusiana na ardhi, kutaongeza tija katika biashara na kilimo na kuwavutia wawekezaji wa ndani ya nchi, wawekezaji wa Kitanzania walioko nje ya nchi na hata wawekezaji kutoka nje ya nchi. Ziko changamoto zinazohusiana na kumbukumbu za ardhi na migogoro ya ardhi ipo mingi pia jambo linalosababisha ofisi za usajili wa ardhi kulemewa na migogoro ya namna hiyo inayosababisha upatikanaji wa taarifa sahihi za ardhi kuwa mgumu na kutolewa kwa wakati. Kwa sababu hiyo, Tanzania imelazimika kutafuta suluhisho la matatitzo hayo kwa kuleta utaalamu wa kisasa wa kuratibu maswala yote yanayohusiana na ardhi.

© 2016 Haki zote zimehifadhiwa | Onyo | RAMANI YA TOVUTI