Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (MLHHSD)

Wizara ya Ardhi hapo awali, ilianzishwa kama idara ya ardhi. Lakini kulingana na shughuli na majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa chini ya idara hii kuwa mengi, idara ya ardhi ililazimika kubadilisha jina na kuwa wizara inayojitegemea. Jina lake la sasa ni Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (MLHHSD) ambapo ni muunganiko wa Idara muhimu kama: utawala wa ardhi, upimaji na ramani, mipango miji na makazi. Vitengo vya msingi zaidi ni kitengo cha Usajili, Tathmini, Ardhi za Wilaya na Mahakama ya Makazi. Sambamba na hivyo vitengo vya msingi, ili kuongeza ufanisi wa kazi Wizarani, Wizara ya Ardhi iliongeza vitengo kama Utawala na Rasilimaliwatu, Fedha na Uhasibu, Ukaguzi wa ndani, Huduma za Kisheria, Sera na Mipango, Habari, Mawasiliano na Technolojia, Habari-Elimu na Mawasilianao na Usimamizi wa Manunuzi.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (MLHHSD) pia inafanya kazi kwa karibu zaidi na mawakala wanaoshughulika na Makazi pamoja na Utafiti wa Vifaa vya Ujenzi, Tume inayohusika na Mipango na Matumizi ya Ardhi na pia Shiraka la Nyumba la Taifa. Wizara ina majukumu na Mamlaka ya kuhakikisha kuna usimamzi sahihi wa matumizi ya ardhi na maendeleo ya makazi ya binaadamu kwa manufaa ya kiuchumi na kijamii kote nchini.

© 2016 Haki zote zimehifadhiwa | Onyo | RAMANI YA TOVUTI