MFUMO UNGANISHI WA TAARIFA ZA ARDHI YAANI ILMIS NI NINI? (ILMIS)

Mfumo unganishi wa taarifa za ardhi yaani Intergrated Land Management Information System (ILMIS) ni mfumo wa kijiographia hususani kwa ajili ya kupata taarifa za kina pamoja na matumizi ya ramani za ardhi. Ni sawa na Mfumo wa Taarifa za Kijiographia "Geographic Information System"; ILMIS iliundwa ili kupata chombo kitakachoweza kusimamia na kutunza taarifa zote zinazohusiana na ardhi katika nchi husika, pia inajumuisha taratibu na utaalamu wa ukusanyaji wa taarifa, kusahihisha, kuandaa na kusambaza taarifa za ardhi. ILMIS ni chombo kamili kilichoundwa kwa ajili ya kujenga, kuona, kuchambua, kuhabarisha na kuchapisha taarifa zinahusiana na ardhi. Kiliundwa pia ili kurahishisha ugawaji wa maeneo, umilikishaji, usimamizi na utoaji wa taarifa za ardhi kwa ujumla. Mbali na hayo, ILMIS inaweza ikajumusha taarifa nyingine za muhimu kama; masuala ya udongo, maji, mvua ama taarifa za kijamii na uchumi.

Kadiri changamoto za undelezaji wa ardhi zinavyoongezeka hususani katika Nchi zinazoendelea, mfumo wa umiliki wa ardhi umeachwa,umekosekana, umetelekezwa au wakati mwingine unasahaulika kabisa; kwa hiyo bado kumekuwa na umuhimu mkubwa wa kuwepo kwa mfumo rasmi utakaoshughulika na maswala yanahusiana na ardhi. Kwa mtazamo huo, nchi nyingi kwa sasa zinautambua na zimeona umuhimu wa kuwa na chombo hichi ambacho kina nguvu kubwa na hakina mizozo yeyote. Utelekelezaji huu wa ILMIS utasababisha kupungua kwa idadi kubwa ya migogoro inayohusiana na ardhi kwa nchi husika; na kwa wakati huohuo kupunguza udanganyifu na rushwa na kupata ardhi ya uhakika isiyokuwa na migogoro na kurahisisha usimamizi na utawala bora kwa walengwa na kuhamasisha uwekezaji. Hatimaye Mradi wa ILMIS umeanzishwa ili kuisadia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo (MLHHSD) kurekebisha mfumo uliopo sasa.

© 2016 Haki zote zimehifadhiwa | Onyo | RAMANI YA TOVUTI